Tarehe 03/07/2023 katika Mahakama ya Wilaya Muleba mbele ya Mh. Daniel Nyamkerya (SRM) , Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Muleba limefunguliwa shauri la Rushwa No. 04/2023 Jamhuri dhidi ya Bw. Asad Burhan Batenga.
Bw. Batenga ambaye ni Afsa Ardhi Halmashauri ya Wilaya Muleba kati ya Oktoba na Novemba 2022 alishawishi na kupokea kiasi cha Milioni moja (1,000,000), kutoka kwa mwananchi, kama kishawishi cha kumpimia ardhi na kumpatia hati za umiliki katika ardhi hizo, hivyo anashtakiwa na Jamhuri na kosa la kujihusisha na vitendo vya rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na (2) katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na kifungu cha 301 na 302 katika Sheria ya Kanuni ya aadhabu Sura ya 16.
Upande wa Jamhuri (PCCB) uliwakilishwa na Daudi Jacob Oringa kwa kumsomea mashtaka mshtakiwa na mshtakiwa kukana mashtaka yake.
Shauri litakuja tena tarehe 14/07/2023 kwa hatua ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.