Tarehe 3 Julai, 2023 ilifunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi Na. 08/2023, katika Mahakama ya Hakimu mkazi Tabora, Jamhuri dhidi ya Beda Mnyaga Nyasira- Mhasibu wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora.
Mshtakiwa amefikishwa Mahakamani kwa kosa la ubadhirifu kinyume na Kif Cha 28 Cha PCCA.
Mshtakiwa aliingia kwenye mfumo wa malipo na kuhamisha kiasi cha shs 21 milioni za Makama Kuu Kanda ya Tabora na kulipa wanaodai mirathi Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara.
Kesi itakuja tarehe 5/07/2023 kwa ajili ya kutajwa.
Mshtakiwa ameonesha nia ya kufanya pleabargain.
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Kesi hii inaendeshwa kwa ushurikiano wa mawakili wa ofisi ya TAKUKURU na Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Tabora.