Juni 30, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mlele mbele ya Mh. Prascovia , Kaimu Hakimu Mfawidhi Wilaya, imefunguliwa kesi Corruption Case No. 79/2023 Jamhuri dhidi ya JACKSON PETRO SHULA Mtendaji wa Kata ya Ilunde ambaye ni mwajiriwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Akisoma mashtaka hayo Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi Bw. Amos Weston Mwalwanda alisema mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo sh. 500,000/- kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA ya 329 marejeo ya 2022 toka kwa Bw. Samike Shilingi Ngasa wa Kijiji cha Ilunde. Kwamba alichukua fedha hizi ili aweze kuwaachia ng’ombe 24 waliokamatwa na kuzuiwa kwa kosa la kuchungwa ndani ya eneo la Shule ya Sekondari Ilunde.
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.