Kesi namba CC.165/2023 imefunguliwa Juni 28, 2023 katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kivukoni iliyopo Kinondoni.
Mshitakiwa ni Bi Devota Devid Mkwawa– Mfanyabiashara mkazi wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Ameshitakiwa kwa makosa ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za kughushi kinyume na vifungu vya 333, 335(a)&(d), 337 na 342 vya Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 Rejeo la 2019.
Amesomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kivukoni iliyopo Kinondoni Mhe. Kaluyenda.
Kesi imeahirishwa hadi Julai 12, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa hoja za awali(PH).
Mshtakiwa atakuwa nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.