Mnamo Juni 28, 2023, Ilifunguliwa Kesi ya Uhujumu Uchumi Na.5 ya 2023 mbele ya Hakimu Mkazi KAVALO, chini ya Waendesha Mashtaka wa Serikali (TAKUKURU) Bw. Fussi na Siriwa
Mshtakiwa ni Sylivester Vananth (Mkusanya mapato wa Halmashauri) akikabiliwa na kosa la Ubadhirifu wa sh. 10,666,600, mali ya halmashauri kupitia mashine ya POS kinyume na kifungu Cha 28(1) PCCA.
Mshtakiwa alisomewa shtaka na kukiri kosa na kisha kuomba nafuu ya adhabu kwamba amekwisha lipa deni lote na kutoa uthibitisho. Pia ameeleza kuwa yeye mgonjwa.
Mahakama baada kuona uthibitisho wa kulipa deni imemhukumu kwenda jela miaka miwili.