Juni 28, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Muleba mbele ya Mh. Mwambeleko, Hakimu wa Wilaya ya Muleba imeamriwa kesi * ya RUSHWA No. 2/2023.
Kesi hii ni ya Jamhuri dhidi ya Mashaka Magesa Ngereja ambaye alishitakiwa kwa kosa la kupokea HONGO Tsh 250,000 kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Mapitio ya 2022 kwa lengo la kuuza sehemu ya eneo la Kijiji cha Kahangaza ndani ya kitongoji cha Kanyamlima Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.
Upande wa Jamhuri (TAKUKURU ) uliwakilishwa na Wakili Kelvin Murusuri
Baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote, iliridhika kutendwa kwa kosa hilo na kumtia hatia mshtakiwa.
Mahakama imemhukumu mshtakiwa kulipa faini ya shs 500,000/= (Laki Tano) au kwenda jela miaka mitatu.
Aidha,Mahakama imemwamuru mshtakiwa kurejesha fedha zote sh. 250,000/- alizochukua kama HONGO na Ardhi iliyouzwa irejeshwe katika Serikali ya Kijiji na kwamba mauziano yaliyofanyika ni Batili.
Mshtakiwa ameenda jela.