Juni 27, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Sikonge mkoani Tabora, limefunguliwa Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 03/2023.
Mshtakiwa ni Nicholaus Magembe ambaye ni mwajiriwa wa kujitolea kama mkusanya mapato katika H/Wilaya Sikonge.
Mshitakiwa ameshitakiwa kwa kosa la ubadhirifu na kuisababishia Halmashauri hasara ya kiasi cha Tzs. 4,514,500/= alizokusanya na kushindwa kuziwasilisha Halmashauri.
Mshitakiwa amekana kosa, yupo nje kwa dhamana na shauri litakuja tarehe 17/07/2023 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.