Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Juni 28, 2023, Jamhuri imeshida kesi ya Jinai yenye namba CC 151/2021 iliyokuwa ikiendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Imani Nitume na Fatuma Waziri.
Katika kesi hii mshitakiwa Habibu Rashidi Mnkumbi aliyekuwa Fundi Sanifu Maabara ya Afya katika Chuo cha Maji Ubungo amekutwa na hatia ya makosa yote mawili ya kughushi vyeti vya kuhitimu Stashahada ya Maabara ya Afya ya Chuo cha KCMC kinyume na kifungu cha 333,335(a) na 337 na kuviwasilisha katika Chuo cha Maji na kupata ajira kinyume na kifungu cha 342 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 pitio la mwaka 2002.
Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa makosa yote mawili na kuamriwa kwenda jela miaka 2.