Juni 27, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Muleba mbele ya Mh. Mwambeleko, Hakimu wa Wilaya ya Muleba imeamriwa kesi ya Jinai No. 1/2023 Jamhuri dhidi ya Stephen Karugendo, Mtendaji ambaye alishitakiwa kwa *kosa la kutotii amri na wajibu halali wa kisheria chini ya kif cha 123 cha Kanuni za Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2022.
Anashtakiwa kwamba, akiwa na POS namba 307600006790, alikusanya mapato ya Halmashauri ya Muleba sh. 8,974,125/- kisha kutoziweka bank, hivyo kukiuka kifungu cha 29 (2) (c) cha Sheria ya Local Government Finance Act Sura ya 290 mapitio ya 2022.
Upande wa Jamhuri (PCCB) uliwakilishwa na Bw. Kelvin Murusuri ambaye aliongoza kesi hiyo na baada ya Mahakama kusikiliza pande zote za shauri, Mahakama iliridhika kutendwa kwa kosa hilo na kumtia hatiani mshtakiwa.
Aidha baada ya maombolezo ya Mshtakiwa, Mahakama imemhukumu mshtakiwa kulipa faini ya *sh Laki mbili au jela miezi sita, kwa kosa hilo la kutotii wajibu wa kisheria wa kuweka au kuwasilisha fedha za Umma Serikalini na pia kupitia maombi ya Wakili Murusuri Mshtakiwa ameamriwa alipe fedha zote sh. 8,974,125/- ndani ya miezi sita.