Shauri la Uhujumu Uchumi namba 32/2023 – Jamhuri dhidi ya TULUSUBYA BUNINI KAMALAMO na WENZAKE 14 ambao ni watumishi wa Halmashauri ya Jiji la DSM, iimefunguliwa Juni 26, 2023 mbele ya Mh. Mazengo (PRM) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wameshtakiwa kwa makosa 143 yakiwemo; Matumizi mabaya ya madaraka, Ufujaji na Ubadhilifu, Kuongoza genge la Uhalifu, Kughushi, Kuingiza taarifa za udanganyifu katika mfumo, Utakatishaji fedha haramu na Kuisababishia Serikali hasara ya shilingi za kitanzania 8,931,598,500/=.
Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama haina mamlaka ya kusikiliza shauri hili kwa sasa.
Kesi imepangwa kutajwa tarehe 10.07.2023 na washtakiwa wamewekwa mahabusu mpaka tarehe ya kesi.