TAKUKURU, ZAECA na TSA WASAINI MoU YA USHIRIKIANO KIKAZI

Juni 26, 2023, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar – ZAECA pamoja na Chama cha Skauti Tanzania – TSA, zimesaini Mkataba wa Makubaliano ya kikazi (Memorandum of Understanding – MoU).

Makubaliano haya yamefikiwa kutokana na ushirikiano uliopo katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hizi (TAKUKURU, TSA na ZAECA), hivyo Taasisi hizi tatu zimeona upo umuhimu wa kuongeza wigo wa ushirikiano hususan katika kuwaelimisha vijana wa Skauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kushiriki kikamilifu katika kuzuia vitendo vya rushwa na vile vya uhujumu uchumi.

Ushirikishwaji huu wa kundi la vijana katika mapambano dhidi ya rushwa ni takwa la kisheria lililotamkwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007. Sheria hii inaitaka TAKUKURU kushirikisha umma wakiwemo vijana katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa.

Taarifa kwa Umma