Juni 23, 2023 imefunguliwa kesi ya Jinai namba CC. 12/2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Tanganyika, mbele ya Mh. Mwakihaba. Jamhuri dhidi ya ADAM PIUS TENDA (Mlinzi ofisi ya Mkuu wa Wilaya ) Wilaya ya Tanganyika, Mkoani Katavi.
Hati ya Mashtaka imesomwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Kelvin Mwaja, kwamba siku ya tarehe 30.05.2023 aliomba kiasi cha Shilingi 40,000/= kutoka kwa Juma Meckson Wilson ili amsaidie kupata cheti chake cha kuzaliwa na Tarehe 30.05.2023 alipokea kiasi cha Shilingi 43,000/= kutoka kwa Juma Meckson Wilson ili amsaidie kupata cheti chake cha kuzaliwa.
Mshtakiwa amejihusisha na vitendo vya Rushwa kinyume na k/f cha 15 cha sheria ya PCCA Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022. Mshtakiwa amekana makosa yake na yupo nje kwa dhamana.