Juni 21, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi No.06/2023 Jamhuri Dhidi ya Bw. Gregory Matandiko, Afisa Manunuzi na Yasini Msangi, Afisa Mipango Miji Wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na ilikuwa Mbele ya Mh. Flora Bhalijuye, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Korogwe Mhe. Shangwe.
Waendesha Mashtaka katika kesi hii, Bi. Sarah Wangwe wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS) akishirikiana na Doreen Kaskazi, Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU, wameieleza Mahakama Kwa Kusoma Hati ya Mashitaka Kwamba, Washtakiwa katika kesi hii, Bw. Gregory Matandiko na Yasini Msangi ambao ni Maafisa Manunuzi na Afisa Mipango Miji mtawalia, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wanakabiliwa na Makosa matano ya Matumizi ya Nyaraka kwa lengo la Kumdanganya Mwajiriwa kinyume na Kifungu Cha 22 Cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022, ikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza pamoja na Kifungu Cha 57(1) na 60 (2) Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 Marejeo ya Mwaka 2022 pamoja na kosa la kuhalalisha Nyaraka za Uwongo kinyume na vifungu vya 342 na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 Marejeo ya Mwaka 2022.
Aidha Watuhumiwa walitenda Makosa hayo kwenye Mchakato wa Manunuzi katika Mradi wa Ujenzi wa Wodi tatu katika Hospitali ya Makuyuni ambayo Ni Hospitali ya Halmashauri Wilaya ya Korogwe.
Washtakiwa Wote Wamekana makosa yanayomkabili na wapo nje kwa dhamana na kesi imehairishwa ambapo imepangwa Tarehe 20.07.2023 kwa Ajili ya Usikilizwaji wa Hoja za awali.