Kikao cha faragha kati ya wawakilishi wa Benki ya Dunia na wanachama wa Shirikisho la Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki – EAAACA, kimefanyika kujadili namna Benki ya Dunia inavyoweza kuingia kwenye makubaliano ya ushirikiano (MoU) kati yake na Taasisi wanachama ikiwemo TAKUKURU. Kikao hiki kimefanyika wakati wa Mkutano wa ‘International Corruption Hunters Alliance – ICHA’, uliofanyika Abidjan – Ivory Coast ambapo Mkurugenzi wa Uchunguzi TAKUKURU Bw. Isdory Kyando ameshiriki.