Juni 16, 2023, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni amemtembelea Balozi wa Palestina nchini Mhe. Balozi Hamdi Mansour AbuAli, ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya TAKUKURU na Mamlaka ya Kupambana na Rushwa ya Palestina, unaotokana na MoU iliyosainiwa na Taasisi hizi mbili zenye jukumu la kuongoza mapambano dhidi ya Rushwa katika nchi zao.