Leo tarehe 20/06/2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, imetolewa hukumu ya kesi ya Jinai No.38/2023 iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi Mhe. Shangwe.
Mshtakiwa katika kesi hii ni Bw. Nassim Mbazu ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipapa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ambaye alikuwa akikabiliwa na kosa la Wizi kwa Mtumishi wa Umma kifungu cha 258 (1) na 270 ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya mwaka 2022
Mshtakiwa alikiri kosa linalomkabili na kutiwa hatiani. Mahakama imeamuru Mshtakiwa kutumikia Adhabu ya kifungo cha nje cha mwaka Mmoja (conditional discharge), adhabu hiyo ikienda sambamba na kutakiwa kurejesha kwa Mwajiri wake Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kiasi cha fedha alichoiba cha Shs. 2,671,300/= ambacho Mshtakiwa amesharejesha.
Waendesha Mashtaka katika kesi hili wakiwa ni Simona Mapunda akishirikiana na Conrad Kabutta.