Juni 07, 2023, katika Mahakama ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe mbele ya Mhe. Irvan Msacky, Shauri la Jinai Namba 40/2022 limetolewa maamuzi kwa mshtakiwa Isaya Samwel Madoki kutiwa hatiani kwa kosa la wizi kwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258(1) na 270 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019.
Hukumu hii ni baada ya kusikiliza mashahidi tisa na vielelezo kumi na nne vya upande wa Jamhuri, huku upande wa utetezi ukiwa na shahidi mmoja na vielelezo Ishirini na sita.
Ilithibitika mahakamani kuwa mshtakiwa ambaye alikuwa ni Mkusanya Mapato alikusanya kiasi cha sh 86,455,360/= na kuwasilisha benki sh 75,820,410/= na hivyo kuiibia fedha Halmashauri ya Makete kiasi cha sh. 12,634,356.
Ilibainika kuwa fedha hizo zilikusanywa na yeye kama Mkusanya Mapato kutoka kwa Watendaji wa Kata za Ipelele, Kitulo, Mlondwe, Kinyika, Isapulano, lniho na Lupalilo.
Mhe. Hakimu Irvan Msacky, amemhukumu mshitakiwa kwenda jela miaka miwili (2) na pindi amalizapo kifungo chake arejeshe kiasi cha fedha alizoziiba sh 12,634,950/= TAKUKURU Njombe, Juni 7, 2023