Juni14, 2023 Mahakama ya Wilaya ya Hai imemtia hatiani fundi Mchñudo wa Tanesco Wilaya ya Hai, Bw.David Kisey kutumikia kifungo cha nje cha miaka mitatu katika kesi ya uhujumu uchumi Na 4.2023
Aidha, Mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa matatu yafuatayo: Matumizi mabaya ya mamlaka, ufujaji na ubadhirifu na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Ameshtakiwa kwa kujipatia kiasi cha shillingi 760,000, akimdanganya mwananchi aliyetaka huduma ya kuunganishiwa umeme kwamba angempatia huduma hiyo, kitendo ambacho kilikuwa kinyume na utaratibu wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO).
Mh. Hakimu Julieth Mawole aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na atatumikia kifungo cha miaka mitatu.
TAKUKURU HAI, KILIMANJARO Juni 14, 2023