Juni 08, 2023 imefunguliwa kesi ya Jinai namba CC. 69/2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mlele, mbele ya Mh. Bilal.
Kesi hiyo ni Jamhuri dhidi ya AMOS GEORGE MAHANGA (Mwenyekiti wa Kijiji )- Kijiji cha Uwanja wa Ndege, katika H/W ya Mlele, Mkoani Katavi.
Hati ya Mashtaka imesomwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Kelvin Mwaja, kwamba siku ya tarehe 09.01.2023 aliomba kiasi cha Shilingi 300,000/= kutoka kwa Marry Msagati ili amsaidie kurejesha mali zake kutoka kwa Hussein Mapula na Tarehe 10.01.2023 alipokea kiasi cha Shilingi 210,000/= kutoka kwa Marry Msagati ili amsaidie kurejesha mali zake kutoka kwa Hussein Mapula.
Mshtakiwa amejihusisha na vitendo vya Rushwa kinyume na k/f cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022.
Mshtakiwa amekana makosa yake na yupo nje kwa dhamana.