Juni 08, 2023 imefunguliwa Kesi ya Uhujumu Uchumi namba ECO. 05/2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, mbele ya Mh. Changwe.
Kesi hii ni ya Jamhuri dhidi ya Jisenge M. Salum (Afisa Mtendaji )ambaye pia ni Mkusanya Mapato kwa njia ya POS katika H/W ya Mbozi, Mkoani Songwe.
Hati ya Mashtaka imesomwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Hilda Mtaki kwamba kati ya tarehe 25.07.2018 na 02.07.2022, Mshtakiwa akiwa na nia ovu alitumia madaraka yake vibaya kinyume na k/f cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022, kwa kushindwa kupeleka fedha kwa mhasibu wa H/W ya Mbozi kiasi cha shilingi 5,849,900/= kinyume na Memoranda namba 37(2) na 50(5) ya Memoranda ya Fedha ya Serikali ya Mtaa ya mwaka 2009 kwa lengo la kujipatia maslahi binafsi.
Pia Mshtakiwa anakabiliwa na shtaka la Ufujaji na Ubadhirifu kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022 ambapo mshtakiwa anadaiwa kati ya tarehe25.07.2018 na 02.07.2022 akiwa Mkusanya mapato katika H/W ya Mbozi alizifanyia ubadhirifu kiasi cha shilingi 5,849,900/= mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi zilizofika kwenye himaya yake akiwa mtumishi wa umma .
Mshtakiwa amekana makosa yake na yupo nje kwa dhamana.