Juni 6, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Lindi, imefunguliwa Kesi ya Jinai Namba 29/2023 dhidi ya SAIDI CHANDE MKINGIE (Afisa Mifugo, Kata ya Matimba, Wilaya ya Lindi), kwa kosa la kushawishi na kupokea hongo k/f cha 15(1) (a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022.
Mshtakiwa aliomba na kupokea kiasi cha sh. Laki Moja (100,000/=) kutoka kwa MURITADHA SAIDI MTENDANGA, ili asimchukulie hatua za kisheria kwa kosa la kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi wa kike.
Mshtakiwa amesomewa Hati ya Mashtaka na kukana kosa lake.
Mshtakiwa yupo rumande kwa kuwa ameshindwa kukidhi vigezo na masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama.
Kesi itakuja tena Juni 19, 2023 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.
Kesi hii inaendeshwa na wakili Fatma Chimbyangu wa TAKUKURU Lindi.