Leo tarehe 15/06/2023 katika Mahakama ya Mkoa – Bukoba, mbele ya Mhe. Massesa– Hakimu Mfawidhi Mkoa, imeamuliwa kesi ya Jinai Na. 6/2022 Jamhuri dhidi ya Mickdad Abdurashid Juma, ambaye alishtakiwa kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo chini ya kifungu cha 29 (3) cha Sheria ya Vizazi na Vifo sura ya 108, mapitio ya 2022, ambapo mshtakiwa alidaiwa kutoa taarifa za uongo ili kupata cheti cha kuzaliwa katika mazingira ya rushwa.
Baada ya ushahidi kutolewa katika shauri hilo, Mahakama iliridhika na kumtia Hatiani mshtakiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo.
Mahama imemhukumu mshtakiwa kulipa faini ya shilingi za Kitanzania Laki tatu (300,000) au kwenda jela kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Shauri hilo liliendeshwa na Mawakili wa Serikali (TAKUKURU) Bw. Kelvin Murusuri akisaidiwa na Daud Jacob.
TAKUKURU Bukoba , Juni 15, 2023