KUTOKA MAHAKAMANI HAI – KILIMANJARO

Mei 29, 2023 Shauri la Uhujumu Uchumi Na 4.2023 dhidi ya Afisa wa TANESCO Bw. DAVID KISEY lilifunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Hai.

Mshtakiwa anakabiliwa na makosa 3 ambayo ni ubadhirifu, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na matumizi mabaya ya mamlaka .

Mshtakiwa akiwa mwajiriwa wa TANESCO kwa vipindi tofauti tofauti mwaka 2022, alijipatia kiasi cha sh. 760,000= kutoka kwa mteja akimdanganya kwamba angempatia huduma ya umeme.

Aidha mshtakiwa amekana makosa yote na yupo nje kwa dhamana.

Shauri litakuja kwa masikilizo ya awali Juni 14.2023.