Leo Mei 31, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Muleba mbele ya Mh. Daniel Nyamkerya, Hakimu Mfawidhi Wilaya imeamriwa kesi Corruption No. 1/2022 Jamhuri dhidi Kelvin Rweyemamu Prosper – Mtendaji ambaye alishtakiwa kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo toka kwa baadhi ya wanufaika wa fidia katika mradi wa bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Tanga, lengo ikiwa ni kuwaandikia barua za utambulisho kwa ajili ya fidia kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na (2) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 239 marejeo ya 2022.
Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa na kumhukumu kutotenda kosa lolote la jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja.TAKUKURU Muleba, Mei 31, 2023