Mnamo tarehe 30.05.2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Momba mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya Mh. Claud Masenjelwa, imeamuliwa kesi No. 03/2023 Jamhuri dhidi ya Emma Katabika – Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Katenjile na Mashaka Mwilenga – Fundi Ujenzi.
Kesi hii ilihusu kosa la matumizi mabaya ya nyaraka kwa ajili ya kumdanganya mwajiri kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.
Mahakama imewatia hatiani Washtakiwa baada ya kukiri kosa na kuwaamuru kulipa faini ya sh. 800,000/= kwa wote wawili au kwenda jela miaka 4 kila mmoja na kutakiwa kurejesha fedha kwa mwajiri ambaye ni Halmashauri ya Mji Tunduma kiasi cha shs. 500,000/=.
Washtakiwa wamelipa faini na kurejesha fedha.