Mei 29, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Jamhuri imeshinda Mashauri mawili yaliyokuwa yakiendeshwa katika Mahakama hiyo.
- Ecc no 2/2022 Leonence Manyila Doto Mtendaji Kata ya Lugubu na wenzake wawili, walishtakiwa kwa kosa la kughushi muhtasari na kuhamisha fedha kiasi cha sh. 7,600,000 kutoka kwenye akaunti ya Kata na kuingiza kwenye akaunti ya fundi badala ya kulipa sh. 600,000.
Washtakiwa wawili waliachiwa huru na Leonence Manyila Ditto amehukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shs 1,400,000.
Hadi tunatoka Mahakamani Mshtakiwa alikuwa hajalipa faini.
- CC No. 3/2022 Andrew Peter Rutabaisha Afisa Elimu na Assistant Returning Officer, Kata ya Mbutu – alifanya udanganyifu kwa kuandaa nyaraka yenye maelezo ya uongo kuonesha kuwa ametumia Sh. 800,000/- kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kupigia kura na Sh. 200,000 kwa ajili ya kukodi viti, meza na vipaza sauti kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Mshtakiwa amehukumiwa kwenda jela mwaka moja au kulipa faini ya sh. 500,000 lakini hadi tunatoka Mahakamani mshtakiwa alikuwa hajalipa faini.