Mei 25, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Kaliua mkoani Tabora, TAKUKURU imewasomea mashtaka washtakiwa wawili wa makosa ya Rushwa kwa Kesi ya Jinai Na. 71/2023.
Washtakiwa hao ni RICHARD MAGANGA, Mtendaji wa Kijiji
cha Imagi, Kata ya Nhwande Wilayani Kaliua pamoja na LAURENT ISAYA SENDU, Mtendaji wa Kata ya Nhwande, Wilayani Kaliua.
Washtakiwa kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa la Kupokea Hongo Kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) na 2 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Cap 329 R.E 2022).
Hongo hiyo ilikua ya jumla ya sh. 3,000,000/= kutoka kwa mwananchi (mkulima na mfugaji) wa Kijiji cha Imagi, Kata ya Nhwande Wilaya ya Kaliua kama ushawishi ili asiweze kuunganishwa na watuhumiwa waliohusishwa na makosa ya kipolisi.
Mshtakiwa mmoja(Laurent Isaya Sendu) yuko nje kwa dhamana na Mshtakiwa mwingine (Richard Maganga) amekosa dhamana baada ya kushindwa kupata mdhamini. Kesi limepangwa kuja kutajwa mnamo tarehe 08/06/2023 .