Leo Tarehe 25/05/2023 katika Mahakama ya Wilaya Liwale mkoani Lindi, amesomewa mashitaka katika Kesi ya Rushwa Na. 01/2023 mshtakiwa SELEMANI FADHILI KHALFANI, Mtendaji wa Kijiji
cha Kimambi, Kata ya Kimambi Wilayani Liwale.
Mshitakiwa anashtakiwa kwa kosa la Kupokea Hongo Kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) na 2 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Cap 329 R.E 2022).
Hongo hiyo ilikua ya jumla ya shs. 2,000,000/= kutoka kwa JOHN CHAMBI KASEKELE ambaye ni mkulima, kama ushawishi ili maombi yake ya ardhi ekari 400 kwa ajili ya kilimo yaweze kujadiliwa katika Kikao cha Serikali ya Kijiji cha Kimambi.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya kukidhi vigezo na Shauri limepangwa kuja kwa kutajwa tarehe 06/06/2023 .