Mei 22, 2023 imefunguliwa Kesi ya Uhujumu Uchumi namba ECO. 04/2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Momba kwa Mhe. Lyon Jamhuri dhidi ya Bw. Kibwana Said Kibwana, Afisa Maendeleo ya jamii katika Kata ya Myunga, Halmashauri ya Wilaya ya Momba, mkoani Songwe.
Mshtakiwa amesomewa Hati ya Mashtaka na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Simona Mapunda, kwamba kati ya tarehe 04.05.2015 na 26.06.2020, Mshtakiwa akiwa na nia ovu alitumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kupeleka fedha kwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi au kuweka kwenye akaunti ya halmashauri ya wilaya ya Momba kiasi cha shilingi 30,428,100/= ndani ya muda uliotakiwa kinyume na memoranda namba 37(2) na 50(5) ya Fedha ya Serikali ya Mtaa ya Mwaka 2009 kwa ajili ya kujipatia manufaa binafsi.
Mshtakiwa amekana makosa yake na alishindwa kukidhi vigezo vya dhamana na hivyo kupelekwa rumande.