Mei 19, 2023 zimefunguliwa kesi 2 za Uhujumu Uchumi – namba ECO. 02/2023 na ECO. 03/2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Songwe mbele ya Mhe. Lugome.
Kesi hizo ni:-
- Jamhuri dhidi ya Bw. Jaston Winfred Mpigauzi, Mtendaji wa Kijiji na
- Jamhuri dhidi ya Bw. Christopher Mshogo ambaye ni Mtendaji wa Kijiji, wote wakiwa ni watumishi wa H/W Songwe iliyoko mkoani Songwe.
Washtakiwa wamesomewa Hati ya Mashtaka na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Simona Mapunda kwamba kati ya Mwaka 2017 na Mwaka 2023, washtakiwa wote wawili walitumia mamlaka yao vibaya kwa kushindwa kuweka fedha walizokusanya kama mapato na kuzifanyia ubadhirifu kinyume na kifungu cha 31 na 28 (1) cha PCCA sura ya 329.
Jaston Mpigauzi alizifanyia ubadhirifu sh.22,212,499/= alizokusanya kama mapato ya H/W Songwe na Christopher Mshogo alizifanyia ubadhirifu sh. 8,693,220.25/=, mali ya H/W Songwe.
Washtakiwa wamekana mashtaka yao na walipata dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana