Katika Mahakama ya Wilaya ya Hai Kilimanjaro, Jamhuri imeshinda Shauri la Uhujumi Uchumi Na 3/2023 dhidi ya Emmanuel Saimon Lukumay ambaye alikuwa akikabiliwa na shtaka la ufujaji na ubadhirifu wa kiasi cha sh. 350,000 k/kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329, marejeo ya 2019.
Mshtakiwa akiwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kware, Kata ya Masama Kusini alijfuja kiasi cha shs 350,000 ambayo ilitolewa na mnunuzi wa shamba la madini ya ujenzi ikiwa ni malipo ya asilimia 10 ya mauzo ya shamba hilo lililouzwa kwa kiasi cha shilingi 3,500,000.
Mshtakiwa baada ya kupokea fedha hizo hakuwasilisha kwa mwajiri wala hakupeleka benki.
Aidha, mshtakiwa amekiri kosa hilo mbele ya Mheshimiwa Julieth Mahole na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 3 jela.
Shauri hilo lilikuwa likiendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Bi. Suzan Kimaro.