Mei 17, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Hai, Jamhuri imeshinda shauri lililokuwa limefunguliwa kwenye mahakama hiyo mnano Mei 17, 2023.
Shauri hilo ni namba EC 21/2023 dhidi ya Mshtakiwa Bw. Lameck Simbo, ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mungushi Wilaya ya Hai. Alishtakiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kuvunja sheria na kujipatia fedha kiasi cha sh 300,000 ikiwa ni mapato ya kijiji kwa mauzo ya shamba kati ya Rafia Kimaro na Elifuraha Judica Kimaro.
Kosa la pili linahusu ubadhirifu wa fedha za kijiji kwa kujipatia manufaa kinyume na kifungu cha 28(1)cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.
Shauri hilo lilikuwa mbele ya Mh. Julieth Mahole na mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 2 jela au kulipa faini.