Mei 17, 2023 imefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba ECO. 03/2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Momba Mhe. Claudia Msenjelwa.
Kesi hii ni Jamhuri dhidi ya Bi. Emma Philemon Katabika, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Katenjele na Bw. Mashaka Tenson Mwilenga ambaye ni Fundi Ujenzi anayeishi Mpemba katika H/Mji wa Tunduma mkoani Songwe.
Washtakiwa wamesomewa Hati ya Mashtaka na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Simona Mapunda akisaidiana na Conrad Kabutta, kwamba kati ya tarehe 28.06.2021 na 29.06.2021 washtakiwa wakiwa na nia ovu ya kumdanganya Mwajiri, walitumia nyaraka zenye maelezo ya uongo wakitaka kuonesha kuwa Mashaka Mwilenga anastahili malipo ya sh 500,000/= kwa kazi ya ujenzi wa madarasa na ofisi ya Mwalimu Mkuu jambo ambalo kwa uelewa wao halikuwa kweli hivyo kwenda kinyume na kifungu cha 22 cha PCCA sura ya 329 marejeo ya 2022.
Washtakiwa wamekana mashtaka yao na walipata dhamana baada ya kukidhi masharti