Mei 16, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Hai, Jamhuri imeshinda shauri lililokuwa limefunguliwa kwenye mahakama hiyo mnano Juni 16, 2022.
Shauri hilo ni namba CC94/2022 dhidi ya Mshtakiwa Bw. Dominick Joseph Mmasi , aliyekuwa Askari Mgambo wa Mahakama ya Wilaya ya Hai, aliye omba na kupokea rushwa ya sh 150,000 toka kwa Athuman Ally Shemganga, ambaye ni Mwananchi aliyekuwa na shauri katika mahakama hiyo.
Shuri hilo lilikuwa mbele ya Mh. Julieth Mahole na amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela au kulipa faini.