Mei 11, 2023 limefunguliwa Shauri la Jinai Namba 103/2023, Jamhuri dhidi ya Imamu Semkiwa aliyekuwa Fundi Ujenzi Katika Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu – Shule ya Sekondari Shambalai, kwa tuhuma za kutenda kosa la Kughushi Nyaraka Kinyume na Vifungu ya 333, 335 (a), 335 (d) (i) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, Marejeo ya Mwaka 2022.
Mshitakiwa amefikishwa mahakamani hapo kufuatia vitendo vya kughushi kwa kusaini nyaraka za Zabuni zenye thamani sh. 6,000,000/- kwa majina ya watu wengine, kinyume na sheria, katika utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Miundombinu Shule ya Sekondari Shambalai.
Mshitakiwa amekana mashtaka yanayomkabili na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Hakimu aliyesikiliza shauri hilo, Mh. Kavumo Masewa ameahirisha shauri hilo hadi Mei 30, 2023, ambapo mshtakiwa atasomewa hoja za awali.