Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, amewataka Watumishi wa TAKUKURU kuwa ‘WATAKATIFU’ na wa mfano wa kuigwa kwa tabia njema ili waweze kuwashughulikia wenye matendo mabaya wakiwemo Wala Rushwa.
Ameyasema hayo Mei 15, 2023 akifungua MAFUNZO YA AWALI YA UCHUNGUZI KWA WAAJIRIWA WAPYA WA TAKUKURU – 2023, yanayofanyika Shule ya Polisi Moshi.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni amewasisitiza Maafisa Uchunguzi 238 wanaofanya mafunzo hayo, kuwa wanapaswa kuzingatia na kufaulu mafunzo ya nadharia na ya vitendo ndipo wafaulu kujiunga na TAKUKURU.
Mafunzo hayo ya miezi mitano yatahitimishwa Oktoba 2023.