Rais wa Seychelles Mhe. Wavel Ramkalawam amefungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa kwa nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika Seychelles. Mkutano huu uliofunguliwa Mei 15, 2023 utahitimishwa Mei 19, 2023 ukiwa na kaulimbiu isemayo ‘Uniting Commonwealth Africa in the fight against corruption’. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye anashiriki mkutano huu ambapo pia atawasilisha mada inayohusu utekelezaji wa Programu ya TAKUKURU – RAFIKI.