Mei 11, 2023 watuhumiwa 6 kati 9 wameshtakiwa kwa makosa ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji fedha haramu.
Washtakiwa hawa wamefunguliwa mashtaka kupitia kesi Na 11/2023 mbele ya Mhe. Hakimu Urio wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Washtakiwa wamewekwa rumande katika gereza la Segerea kufuatia kuwako kwa makosa ambayo hayana dhamana.
Uchunguzi unaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine 2 pamoja na mali zao.
Inadaiwa kuwa katika kipindi cha Sept 2022 washtakiwa kwa kutumia Kampuni ya Steca Export Co. Ltd, walifanya biashara ya kuuza Madini ya Copper yenye thamani ya sh. 1.6 Bilion kwa Kampuni ya Zhejiang Afol ya nchini China.
Kwamba washtakiwa walisafirisha chupa tupu za vinywaji (wine beverages bottled) badala ya Madini ya Copper, waliyomuuzia mlalamikaji kupitia Clearing Agent ya Mwikolo Logistic & Globvest Group Ltd.
Imethibitika kwamba chupa tupu zilisafirishwa kwa makontena 5 kwenda China kupitia wakala wa meli MAERSK.