Mei 10, 2023 Mahakama ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, yamefunguliwa mashauri mawili ya Uhujumu Uchumi kama ifuatavyo÷
- ECO 5/2023 dhidi ya PASKALIA JANUARY MSAFIRI ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji ambaye anashitakiwa kwa kosa la ubadhirifu wa fedha za makusanyo ya tozo ya faini kiasi cha shilingi 500,000/= alizokusanya kutoka kwa mfugaji aliyeingiza mifugo kinyume na utaratibu pasipo kuwasilisha kwenye Hazina ya Halmashauri (W)-Chunya.
Mshitakiwa huyo baada ya kisomewa shitaka amekana na amefanikiwa kupata dhamana.
Shauri litaendelea tarehe 18/05/2023 kwa kusoma maelezo ya awali au usikilizaji wa hoja za awali.
- ECO 6/2023 dhidi ya EUSEBIUS GEORGE MIHAYO ambaye ni Afisa Mtendaji Kata na anashitakiwa kwa makosa ya ubadhirifu na wizi kwa mtumishi wa umma.
Makosa haya aliyafanya mara baada ya kutowasilisha makusanyo ya ushuru wa mazao kiasi cha shilingi 5,269,875/= kwenye akaunti ya mapato ya Halmashauri (W) – Chunya.
Mshitakiwa amekiri kosa na mahakama imepanga shauri hili lije tarehe 12/05/2023 kwa ajili ya kutoa hukumu.
Mshitakiwa amewekwa mahabusu hadi tarehe hiyo.