Mei 9, 2023, katika Mahakama ya Wilaya ya Handeni, limefungua Shauri la Rushwa Namba 01/2023 Jamhuri dhidi ya Hassan Mbaruku Mkomwa, Mwenyekiti wa kijiji cha Turiani.
Mshtakiwa amefikishwa Mahakamani hapo kwa kosa la kushawishi, kuomba na kupokea rushwa ya sh. 300,000/=, kinyume na Kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329, Marejeo ya Mwaka 2022.
Mshtakiwa aliomba fedha hizo kwa lengo la kumsaidia mtoa taarifa kumtoa ndugu yake aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Handeni.
Aliposomewa mashtaka yanayomkabili, mshtakiwa amekana makosa yake. Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Mhe. Munga Sabuni, aliahirisha Kesi hadi Mei 23, 2023 ambapo kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa. Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana.