Mei 9, 2023 katika Mahakama ya Wilaya – Handeni mkoani Tanga, limefungua Shauri la Rushwa Namba 02/2023, Jamhuri dhidi ya Said Bakari Hossein, Dereva, mwajiriwa wa Benki ya CRBD.
Mshtakiwa amefikishwa mahakamani hapo kwa shtaka la kushawishi, kuomba na kupokea rushwa ya sh.150,000/= kutoka kwa mwananchi ambaye ni mteja wa Benki ya CRBD na pia mnufaika wa fidia katika Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki – EACOP.
Fedha hizo ni kwa madai kwamba atamsaidia kuharakisha uingizwaji wa fedha za fidia katika akaunti ya mwananchi huyo iliyopo katika Benki ya CRDB tawi la Handeni, kosa ambalo ni kinyume na Kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329, Marejeo ya Mwaka 2022.
Mshtakiwa amekiri makosa yote mawili baada ya kusomewa mashtaka na Hakimu Mhe. Munga Sabuni na hivyo kutiwa hatiani.
Mshtakiwa ameamriwa kulipa fine ya sh. 500,000/= kwa kila kosa, sawa na sh.1,000,000/=.
Mwendesha Mashtaka katika Kesi hii alikuwa Bw. Bernard Ndamalya kutoka TAKUKURU.