Mei 8, 2023, katikati Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe, limefunguliwa Shauri la Jinai Na. 16/2023 Jamhuri dhidi ya Bw. Jackson W. Mahali ambaye ni Mfanyabiashara.
Mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo TRA ili kuhamisha umiliki wa magari kwenda kwake.
Mshtakiwa amekana mashtaka yake yote na amepelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana.
Shauri limepangwa kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikilizwa Maelezo ya Awali (Phg) tarehe 22/05/2023.
Mfanyabiashara huyo ni mkazi wa mjini Mbeya na alikuwa akiendesha biashara za ukopeshaji fedha pasipo kusajiliwa mjini Mbeya, kitendo ambacho ni kosa la Jinai lililomtia hatiani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya mnamo Mwezi Disemba 2022.