Katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2023, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga ameipongeza na kuishukuru ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Rukwa kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii. Katika kulithibitisha hilo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amekabidhi Cheti cha Pongezi kwa Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa Bw. Owen Jasson. TAKUKURU Rukwa Mei 01, 2023.