UZINDUZI WA JENGO LA TAKUKURU LIWALE

“Mradi huu wenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 181 ni mali ya Watanzania wote, hivyo wananchi wa Liwale ninawasihi tuzitumie ofisi hizi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa bila woga ili zifanyiwe kazi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Intelijensia TAKUKURU Mha. Malimi Magembe Mifuko, wakati akisoma Taarifa ya Mradi wa Ujenzi kwa Wananchi walioshiriki hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya TAKUKURU (W) Liwale, Lindi Aprili 27, 2023.