“Nimelikagua jengo hili na nimeridhika kuwa limejengwa kwa viwango vya hali ya juu. Ninaamini Eng. Mganga (RBC) anajua vizuri standards zangu. Hivyo ninawapongeza sana TAKUKURU kwa usimamizi wenu mzuri na kwa kuonesha mfano kwa Taasisi nyingine za Umma na Watanzania, namna ya kusimamia miradi inayotekelezwa kwa force account”. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Lindi, Mhe. Zainab Rajab Telack, wakati akiwahutubia Wananchi wa Liwale kwenye uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya TAKUKURU (W) Liwale. Aprili 27, 2023.