JENGO LA TAKUKURU LIWALE LAZINDULIWA

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Rajab Telack (wa tatu kulia) amezindua rasmi Jengo la Ofisi ya TAKUKURU (W) Liwale mkoani Lindi. Akihutubia kabla ya uzinduzi huo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka Watumishi wa TAKUKURU Wilaya ya Liwale kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa na kuhakikisha kuwa kero dhidi ya rushwa inatoweka wilayani humo. Wakishuhudia uzinduzi huo wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Intelijensia TAKUKURU Mha. Malimi Mifuko na wa kwanza kushoto ni Mha. Abnery Mganga, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi. TAKUKURU Liwale, Aprili 27, 2023.

Taarifa kwa Umma

MSHAURI WA WAFANYABIASHARA (TCCIA ) – MANYARA HATIANI KWA KUGHUSHI