Aprili 25, 2023 Imefunguliwa Kesi
ECC. Na. 01/2023 Mshtakiwa HUSSEIN SALUM NYEMBA (Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji IGUWASA), kwa kosa la kujipatia manufaa kinyume na k/f 23(1)(a) PCCA Sura ya 329 R:E 2019, vikisomwa pamoja na paragrafu ya 21 jedwali la 1, kifungu cha 57(1) na 60(2) Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura 200 Marejeo ya 2019,
Mshtakiwa anashtakiwa kwa kupokea manufaa ya shs. 4,000,000/ kutoka kwa Mfanyabiashara wa mabomba ya maji na viunganishi, baada ya kudai fedha hizo ili afanye malipo ya fedha ambazo Mfanyabiashara huyo anaidai IGUWASA.
Kesi itakuja tarehe 16/5/2023 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali na Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.