KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA YA MBULU – MANYARA

Aprili 25, 2023, Mahakama ya Wilaya ya MBULU imemtia hatiani Mshtakiwa Bw. SAMWEL QAMBINA DUKHO, katika Shauri la Uhujumu Uchumi Na.06/2022.

Shauri hili lilikuwa mbele ya Mh. Victus KAPUGI na liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka MARTINI MAKANI

Katika shauri hilo mshtakiwa alikua anashtakiwa kwa makosa matatu.

I) Ubadhirifu k/f 28(1) PCCA ambapo kahukumiwa miaka 20 jela.

II) Matumizi mabaya ya madaraka k/f cha 31 cha PCCA ambapo kahukumiwa miaka 20 jela.

III) Wizi katika utumishi wa Umma k/f cha 265 cha Kanuni ya Adhabu ambapo kahukumiwa mwaka mmoja jela.

Mshtakiwa ataitekeleza adhabu hiyo kwa pamoja (concurrently) na Mahakama imemtaka Mshtakiwa kurejesha fedha shs. 3,687,000/= ambazo alizifanyia ubadhirifu au mali yake iuzwe ili kufidia deni hilo.

TAKUKURU- Mbulu, MANYARA. Aprili 25, 2023

Taarifa kwa Umma