Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego (wa pili kulia), amezindua Jengo la Ofisi za TAKUKURU Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, lenye thamani ya Shilingi milioni 186. Mhe. Dendego ameipongeza TAKUKURU Mkoa wa Iringa kwa utendaji kazi wenye tija uliosaidia kuokolewa kwa fedha nyingi za Serikali. Akitoa Maelezo ya Mradi wa Ujenzi, Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa TAKUKURU Bi. Joyce Shirima (wa pili kushoto) amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha taasisi kupata majengo ya ofisi na kuongeza ari ya watumishi katika utendaji kazi. TAKUKURU Iringa. Aprili 25, 2023.