Aprili 24, 2023 Mahakama ya Wilaya Newala mkoani Mtwara imemtia hatiani mtumishi wa Idara ya Afya Bw. DEODATUS DAUDI MWAMWALA aliyekuwa Tabibu wa Kinywa na Meno katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Newala.
Bw. Mwamwala amehukumiwa kifungo cha Mwaka Mmoja na Miezi Sita JELA Katika Shauri Na. 38/2022 lililokuwa likiendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Bw. SAIDI NG’ANZO, chini ya Mheshimiwa Hakimu Mfawidhi Mwandamizi INNOCENT SOTTER.
Awali mshitakiwa aliomba na kupokea rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyekwenda hospitalini hapo kung’olewa jino, kitendo ambacho ni kosa chini ya kifungu cha 15(1)A cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 marejeo ya 2022.